LIPULI INADAIWA ZAIDI YA TSH. 60M
:
Lipuli FC ipo katika wakati mgumu baada ya kukumbwa na deni la zaidi ya Tsh. 60m kutoka kwa wadau walioisaidia wakati ikiwa ligi daraja la kwanza.
:
Deni hilo limedumu tangu mwaka 2015 ambapo mahakama iliamuru Lipuli iwalipe wadai wake lakini imeendelea kukaidi.
:
Wakili wa wadai amesema: “Wateja wangu wamekuwa na madai dhidi ya timu ya Lipuli ya Iringa. Timu hii ilikuja kuweka kambi mjini Mafinga mwaka 2015, walikaa pale karibu mwezi mzima na waliomba huduma ya chakula kutoka kwa Tunte na huduma ya malazi kutoka kwa Ernest Lusangira.”
:
“Walitoa ahadi kwamba watalipa baada ya muda lakini hawakufanya hivyo wakaondoka na deni ambalo wamekuwa nalo hadi leo.”
:
“Walipaswa kumlipa mama huyu (Tunte) pamoja na kesi zai ya Tsh. 33m kwa upande wa Lusangira walipaswa kumlipa zaidi ya Tsh.30m. Walipelekewa amri ya mahakama ya kulipa deni hilo lakini wakakaidi.”
:
Wakili huyo amesema kutoka na klabu ya Lipuli kukaidi kulipa deni, amepeleka ombi mahakama itoe amri ya kuwakamata viongozi ambayo tayari wameipata kwa hiyo viongozi wa Lipuli wanaweza kukamatwa wakati wowote.
:
Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Lipuli Ayubu Kiwelo amesema hawezi kuzungumza chochote hadi atakapokutana na wahusika.
:
“Tunaambiwa ni deni la mwaka 2015, sisi tumeingia madarakani mwaka jana mwezi wa 7 na hukumu ilitolewa mwezi wa 6 mwaka jana kabla hata hatujaingia madarakani kwa hiyo siwezi kuongea chochote juu ya hilo hadi tukunae na wahusika kujua deni hilo lipoje”-Kiwelo.