Tottenham: DELE ALLI Atakuwa Fiti kuwavaa MANCHESTER CITY

– Kocha mkuu wa klabu ya Tottenham, Mauricio Pochettino Amesema kuwa anaamini kiungo wake Dele Alli atakuwa fiti mpaka siku ya jumatatu kwa ajili ya kuivaa Manchester City, Muingereza huyo Amerejea Katika Mazoezi kamili ya Klabu yake na huenda akapangwa Katika Kikosi cha Klabu yake kitakachowavaa Mabingwa hao Watetezi wa Premier League.
.
– Kiungo huyo alikuwa Nje ya Uwanja akiunguza maumivu ya misuli Mpaka kupelekea kukosekana Katika mechi za Premier League ambazo ni Dhidi ya Watford, Huddersfield, Cardiff na West Ham, pia alikosa mechi tatu za Champions League ambazo ni dhidi ya Barcelona, Inter na PSV.
.
– Alli amecheza mechi Sita tu za Michuano yote Kwa Klabu yake na kafanikiwa kufunga Magoli mawili tu Dhidi ya Newcastle Katika Premier League na Dhidi ya Watford Katika EFL Cup – Siku ya Jumatatu tutashuhudia kiungo huyo akirejea wakati vijana wa Pep Guardiola watakapotembelea Wembley.
.

– Baada ya mechi dhidi ya City, Spurs wataivaa West Ham kwenye Carabao Cup kisha Wolves Katika Premier League na baadae watarejea Katika anga za Ulaya kwenye Champions League Dhidi ya PSV.