BREAKING NEWS: Ndege ya mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha imeungua baada ya kugonga pembezoni mwa uwanja wa King Power Stadium.
Mashuhuda wanasema ndege hiyo aina ya Helikopta iliyumba wakati inajiandaa kuondoka kisha ikalipuka.


Mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu waliokuwamo ndani. Inasemekana mtoto wa bosi huyo ndiye aliyekuwa akiitumia ndege hiyo mara kwa mara. Tukio hili limetokea mara baada ya mchezo kati ya Leicester City na West Ham kukamilika [1-1]. Bosi huyo wa Leicster ana Utajiri wa £5 bilioni. Taarifa pia zinadai huenda bosi huyo alikuwamo ndani ya ndege hiyo.
