Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ametoa ruhusa kwa wachezaji wake wawili, Marcel Kaheza na Mohammed Rashid kutolewa kwa mkopo dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwishoni mwa wiki hii.
Wachezaji hao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba kutokana na uwepo wa ushindani mkali wa namba unaosababishwa na ubora wa wachezaji kikosini.
Klabu ya Singida Unuted imeonyesha nia ya kutaka kuwachukua wachezaji wote wawili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ambacho kimekimbiwa na wachezaji wengi kutokana na ‘ukata’
Tanzania Prisons ilikuwa timu ya kwanza kujitokeza ikimtaka mshambuliaji wao wa zamani Mo Rashidi aliyeifungia timu hiyo mabao 10 msimu uliopita
Simba imedhamiria kuimarisha kikosi chake wakati wa dirisha dogo la usajili huku ikipanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji waliokosa namba ili kulinda viwango vyao