Baada ya kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Burundi, kikosi cha timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania U23 kesho kinatarajia kushuka dimbani kuumana na Azam FC.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa saa moja usiku katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.
Akizungumzia kuhusu mchezo huo, Meneja wa Azam FC, Philipo Alando amesema mchezo huo una umuhimu kwa vijana wa Stars U23 na Azam Fc pia.
Tanzania U23 inajiandaa na mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 dhidi ya Burundi ikiwa tayari iko nyuma kwa mabao 2-0.
Mchezo huo utapigwa Jumanne ijayo, Novemba 20 2019
Kwa upande wa Azam Fc ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.