Yanga 1-2 Sumbawanga Fc | Mechi ya kirafiki

Kikosi cha Yanga kimepoteza mchezo wa kirafiki leo baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Sumbawanga United kwenye mchezo uliopigwa dimba la Mandela

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Thabani Kamusoko kwenye dakika ya 40.

Mchezo huo ulikuwa maalum kwa ajili ya wakazi wa Sumbawanga ambao kwa muda mrefu hawajashuhudia timu zinazoshiriki ligi kuu.

Yanga inatarajiwa kurejea mkoani Mbeya tayari kwa safari ya kurudi jijini Dar es salaam.

Jumapili Disemba 09 itacheza na Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.