Droo: Fainali za AFCON 2019 U17

Droo ya upangaji makundi ya michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 imefanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Tanzania itakayokuwa mwenyeji wa michuano hiyo, imepangwa kundi A sambamba na Angola, Nigeria na Uganda.

Tanzania itafungua michezo ya kundi A kwa kucheza na Nigeria wakati Angola itapepetana na Uganda wakati upande wa kundi B Guinea itaanza kwa kuchuana na Cameroon huku Morocco ikipepetana na Senegal