Kulingana na taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo, mabadiliko hayo huenda yakaanza kutumika kuanzia msimu ujao
Maeneo yaliyoguswa na mabadiliko hayo
1. Pigo la Mkwaju wa Penati
Iwapo mkwaju wa penati utaokolewa na kurudi uwanjani au kugonga mwamba, haitaruhusiwa kupiga tena. Yaani hakutakuwa na nafasi ya kuufuata mpira kujaribu kufunga kwa mara nyingine
2. Goli la mkono
Goli litakalofungwa ambalo litagusa mkono wa mfungaji iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi halitakubaliwa
3. Mabadiliko ya mchezaji
Mchezaji anayefanyiwa mabadiliko sasa taruhusiwa kutokea upande wowote wa uwanja
4. Kuanzisha mpira uliotoka langoni
Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.
5. Kadi kwa makocha
Makocha na wasaidizi wao watakuwa wakipewa kadi za njano na nyekundu kulingana na makosa wanayofanya wakiwa benchi. Kadi hizo zitakuwa na athari ya kukosa michezo kama ilivyo kwa wachezaji
6. Ukuta wa kuzuia mipira iliyokufa (freekick)
Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa ambapo wanaweza kujichanganya ili kuharibu mpangilio wa wapinzani wao
7. Mlinda lango katika kuzuia Penati
Mlinda lango anaruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na mwingine akaweka popote , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari kabla ya mkwaju wa penati kupigwa