Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala wakiongozana na viongozi wengine wa Wizara na TFF, leo wametembelea ukarabati wa uwanja wa Uhuru ambao utatumika Kama uwanja wa mazoezi kwenye michuano ya Total Afcon U17 itakayofanyika kuanzia Aprili 14-28, 2019 Tanzania ikiwa mwenyeji..

