Makonda ‘amtuza’ Manula

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Simba, amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa hatua waliyofikia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Simba ilitolewa kwenye michuano hiyo jana katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa mabao 4-1 na TP Mazembe

Makonda amesema matokeo hayo hayapaswi kuwavunja moyo bali iwe chachu ya kutafuta mafanikio zaidi

Aidha Makonda amempongeza mlinda lango namba moja Aishi Manula kwa kazi kubwa aliyofanya kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe akiahidi kumpa zawadi

“Najua matokeo ya leo (jana) yatatupa tabu sana mtaani ila wewe (Manula) umekuwa nyota wangu ukifika tu DSM njoo uchukue zawadi yako,” amesema

“Watani zangu Naomba mjuwe hatua tuliyofikia ni kubwa sana na hakika Simba inastahiri kupongezwa na Usku nitakuwepo Airpot kuwapokea Makamanda na wapambanaji wetu Simba”