KELVIN JOHN BADO ANANG’ANG’ANA NA UFUNGAJI BORA AFCON U17

Licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa katika kusaka nafasi ya ufungaji bora wa mashindano ya AFCON U 17 yanayoendelea Nchini, Mshambuliaji wa Serengeti Boys Kelvin John ‘ Mbappe’ amesema mpango wake wa kuibuka kinara wa mabao katika mashindano hayo bado upo pale pale hivyo atahakikisha anapambana ili kutimiza ndoto yake
.
.
Ikumbukwe kuwa Nyota huyo alifunga bao moja katika mchezo wa kwanza wakati Tanzania ikipoteza kwa mabao 4-5 dhidi ya Nigeria huku Edimond John wa Serengeti Boys na Wisdom Ubani wa Nigeria wakifunga mabao mawili kila mmoja na kuongoza katika msimamo wa orodha ya wafungaji.
.
.

Mbali na hilo Kelvin amesema kwasasa wanajipanga kufanya vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo ujao dhidi ya Uganda utakaopigwa Jumatano hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
.
.
@officialjamesmlaga