Kocha wa Ac Milan Gennaro Gattuso ajiudhulu

– Klabu ya AC Milan Imethibitisha kuwa, Gennaro Gattuso ameachana Rasmi na klabu hiyo Kama kocha Mkuu kwa Makubaliano maalumu; Gattuso ameiongoza Milan tangu Novemba 2017, uhamuzi huo kautoa Baada ya Klabu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Michuano ya @championsleague msimu ujao, wakimaliza nafasi ya tano katika Msimamo wa Serie A na kuangukia @europaleague.

.

– Gattuso 41; alisema hatma yake atatoa Baada ya Ligi kumalizika Baada ya game yao dhidi ya SPAL wakishinda 3-2, lakini ushindi wao haikuwafanya kuwashusha Wapinzani wao Inter Milan pamoja na Atalanta waliokuwa wakiwania nao nafasi mbili zilizosalia ukitoa Juventus na Napoli walijihakikishia kufuzu kwa muda mrefu.

.

– Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim na kocha wa Lazio, Simone Inzaghi, Sasa wanatajwa kuchukua huenda mmoja wao akatua San Siro; Kwa Kuongeza, Milan Imethibitisha Kwa Mkurugenzi wao wa Michezo, Leonardo nae ametimka Baada ya msimu mmoja kudumu Klabuni hapo.. Anatajwa kutimkia Paris Saint-Germain ambako amewahi kufanya kazi hiyo kabla ya kutua Milan.

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Leave a comment