Tuongee kuhusu soka na Kagawa ..kuelekea fainali ya Europa leo

KUELEKEA FAINALI YA UEFA EUROPA LIGI. 

       Leo kuelekea fainali ya ueropa ligi baina ya arsenal na chelsea nimeona nichambue vikosi vyote viwili na kuzipa asimia zao kuelekea fainal hiyo ya kukata na shoka kwasababu vilabu hivyo vinajuana vilivyo maana vimekutana sana katika mshikemshike wa ligi kuu ya uingereza. 

Chelsea

  Wamemaliza ligi vizuri kwa kufika top four ambapo awali katikati mwa ligi walilega lega sana hadi mashabiki wake kuwa na shaka na timu yao kufika top four hila walibadilika wakarudi vizuri hadi kumaliza ndani ya top four,  pamoja na hayo chelsea kama timuhawapo vizuri kuelekea fainal hii sababu ya majerui aliokua nao mfano kiungo tegemezi mkabji wa chelsea ngolo kante ana hati hati ya kukosa mchezo huo kutokana na majeraha,  hii inatosha kuonesha chelsea kwa kukosena kwa ngolo kante litakua tatizo kubwa kwao,  suala jingine chelsea hawana streika wa kat asilia ambaye yupo fomu ya kufunga, wanae top class streika gonzalo higuain hila hayupo katika fomu yake toka ajiunge na chelsea hivyo naona tumain lao lipo kwa giroud ambaye ni moto hasa katika mashindano haya ya ueropa,  na endapo kocha akamuini giroud ambaye akili yake ipo vizuri sana katika europa anaweza saidia chelsea katika fainal hiyo,  pia suala la kocha wa chelsea kutamka hazarani kua ameshindwa kunyanyua morali ya wachezaji wake na anataka kuipa mkon kwaher klabu hiyo, hii inaonyesha ni kiasi gani chelsea haipo sawa kuelekea fainal hiyo, vilevile kunataarifa za chini chini kulitokea ugomvi baina ya wachezaji jambo ambalo naona linawavuruga sana hasa katika kipindi hiki kuelekea fainali ya ueropa. 

Nguvu pekee waliokua nayo chelsea naona hipo kwa streika wao eden hazard ambaye yupo fomu kweli kweli,  juzi tuu ametoka kupokea tuzo ya mchezaj bora wa msimu aliyechaguliwa namashabiki,  hivyo morali yake hipi juu sana kuelekea fainali hiyo, pia suala lake la kuondoka katika clabu hiyo litampa nguvu yakutaka kuwaacha na kikombe cha ueropa kama zawadi yake kwa mashabiki,  hivyo chelsea tumaini lao pekee naona ni eden hazard na namuona ni mchezaji anayeweza kuamua fainali hiyo.  Mi naipa asilimia 40% chelsea kubeba kombe hilo

Arsenal

      Hawakumaliza ligi vizuri hasa baada ya kikosa nafasi ya top four hila katika kuelekea mwishoni mwa ligi arsenal waliwekeza nguvu zao katika kombe hili la ueropa ambapo wamefanikiwa kufika fainali hivyo naona arsenal wapo vizuri kiakili kuelekea fainali hii ya ueropa ligi,  udhaifu wa arsenal nauona katika beki yao abayo naona wanakosa kiongozi kama david luis,  sergio ramos pale madrid,  vincent kampany pale city. Hivyo arsenal kama watashindwa kucheza vizuri katika beki nayo namuona hazard atawafanya atakachojisikia,  pia suala la kuwakosa aron ramsey kiungo hatari sana kaika kufunga na kusaidia wezie kufunga litakua pengo kubwa kwao pia kumkosa mikhtarian nalo litakua pengo kwao katika ubunifu katika final third yao,  faida waliokua nayo ni streika wao wawili pierre aubemiyang na lacazzete,  wapo vizur sana hawa jamaa na wanaushikiano mzuri sana akikukosa mmoja mwingine anakufunga hivyo arsenal watakua hatari sana hasa eneo la mbele.  Pia suala la kuingia uefa kwa mgongo wa nyuma kwa kuchukua ueropa ligi, nahisi litainua hamasa kwao na kuona tumaini pekee ni kujituma na kupata tiketi ya kushiriki uefa msimu ujao, hivyo arsenal watakua na morali sana ukiongezea na ubora wa washambuliaji wao. Arsenal nawapa asimlia 60 kuchukua kombe hilo.  

Hila mchezo wa fainali ni fainali tu haungaliagi huko fomu kiasi gani kushinda mchezo huo kwani wachezaji ujituma sana kuipa heshima mchezo huo,  hivyo naona utakua mchezo mzuri sana ambaye shabiki yoyote wa soka hatotaka kuhukosa. 

Kagawa10

Leave a comment