KUNDI B:
CHELSEA NA ARSENAL MJIANDAE KUMPOKEA HARY KANE
Tottenham msimu UCL wanaelekea kupoteza dira. Wana alama 1 tu. Msimu uliopita katika michezo 6 walishinda 5 na kutoka sare mmoja. Tena walifanya maajabu kwa kumfunga Real Madrid aliyekwenda kutwaa ubingwa mabao matatu. Katika michezo 6, walishinda mabao matatu katika michezo minne.
Msimu huu katika michezo mitatu wanadaiwa mabao matatu. Wamefunga mabao matano wameruhusu manane. Aibu. Hili kundi bado ni gumu sana kwa Inter pamoja na Tottenham katika kupata nafasi ya kusonga mbele.
Tottenham mchezo ujao anakutana na PSV, Tottenham wanapaswa kushinda mchezo huo ili angalu wafikie alama 4. Inter anazo alama 6. Inter ana wakati mgumu kidogo kumfunga Barcelona akiwa kwake ingawa anahitaji hata sare. Inter kama watafungwa watabakiwa na alama zao 6 kama atashinda watapa alama 9 na hii itakuwa balaa zaidi kwa Tottenhan. Lakini faida kubwa waliona nayo Inter watawakaribisha PSV vibonde nyumbani. Hapo watahitaji alama 3 ili wafikishe alama 9. Wakati huo Tottenham atakuwa Camp Nou kama wakifanikiwa kutoka salama basi wakatoe sadaka.
Safari ya Tottenham kufuzu inatiwa dosari na shimo la Camp Nou. Mbaya zaidi Inter watawasubiri Barcelona Guissepe de Meazza kwa hiyo uwezekano wa kuambiwa sare upo. Faida pekee wanayotegemea Tottenham ni mchezo wao wa mwisho na Inter kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kwa mawazo yangu Tottenham yupo kwenye wakati mgumu zaidi na bila shaka Chelsea na Arsenal wote kwa pamoja kwa mikono miwili wampokee ndugu yao kutoka London. Hivyo wajiandae kisaikolojia kumkaba Harry Kane.

#UCL Tottenham #hawatoboiii