UEFA : PSG wakiendea hivi Hawatoboi

KUNDI C:
PSG WAKIENDELEZA MPIRA WAO WA KUPAKA PODA HAWATOBOI

Liverpool alama 6, Napoli alama 5, PSG alama 4. Hivi Neymar ataficha wapi sura yake na pesa zote zile alizonunuliwa takribani Paund 222M kama ikitokea wametolewa hatua ya makundi?

Kama kuna kundi gumu mwaka huu basi hili kundi ni la kukata na shoka. Huyu Napoli kama Masikhara vile anaweza akashangaza wengi licha ya kutopewa nafasi kabisa. Tusishangae kuona hawa matajiri wakirudi mtaani kwao kucheza na watoto wenzao huko league 1.

Nahisi mchezo ufuatao wa Napoli na PSG ndio utakaotoa dira haswa kwamba tuendelee kusubiria mvua iishe au tutoke na mwamvuli.

Nafasi ya PSG kusonga mbele bado ipo, Nafasi ya Napoli vivyo hivyo, Liverpool ndo kwanza yupo kilele.

Mpaka sasa PSG na Barcelona ndio timu zilizofunga mabao mengi [10] kwa hiyo lolote laweza kutokea. PSG wana mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool pale Parc des princess nahisi kwa mchezo waliocheza mechi iliyopita kama hawatabadilika basi wanaweza kupigwa nje ndani, lakini Napoli watakaribishwa Anfield. Najiuliza hapa inawezekana Napoli wakatibua vibe lote la Majogoo pale Anfield kweli? Napoli mpaka sasa katika mechi 3 wamefunga mabao 3, bado kwa takwimu hizi ni ngumu sana kumwekea dhamana kupata ushindi pale Anfield kirahisi.
Mechi iliyobakiwa kwa PSG kukata tiketi ni Belgrade ambayo nina amini hata kama itachezwa Kinesi PSG atashinda sio chini ya bao 3.

Uwezekano wa yeyote kati ya Liverpool na PSG au Napoli kutolewa bado upo wazi hasa ukitazamia wote wamepishana alama 1 tu huku michezo ikibakia mitatu.. #UCL Ila hapa PSG wakiendeleza ubishoo #hawatoboiii