Bao la FEI TOTO Lampa mtonyo

Goli la Fei Toto dakika ya 90 dhidi ya KMC kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara lampa mtonyo kutoka kwa mashabiki wa Yanga.
:
Ilikuwa ni aina ya mechi ambayo inaitangaza vyema ligi yetu kwa sababu ilikuwa na utamu mwanzo hadi mwisho haikuwa mechi iliyoegemea upande mmoja.
:
Mechi ilikuwa kinyume na matarajio ya wengi ambao walikuwa wanajua Yanga itashinda lakini kilihokuwa kinasubiriwa ni kuona itashinda magoli mangapi.
:
Pamoja na Yanga kushinda lakini haikuwa rahisi, KMC walitoa changamoto ya hali ya juu kutokana na wachezaji ilionao kama Kaseja, Ally Ally na wengine.