Brasil vs Cameroon November 20 : HAPATOSHI

– Hapatoshi jijini London Novemba 20, The Indomitable Lions “Cameroon” uso kwa uso dhidi ya Mabingwa Mara tano wa Dunia “Brazil” katika mechi ya kirafiki.

.
– Shirikisho la Soka Nchini Brazil limethibitisha kuwa November 20 watashuka Dimbani kukipiga Dhidi ya Cameroon, zitakuwa zimepita siku Nne baada ya Cameroon kutoka kucheza mechi Dhidi ya Morocco Katika mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2019 wao ndio watakuwa Wenyeji.
.
– Cameroon Wakiwa wao kama wenyeji wa fainali kubwa Barani Afrika hapo mwakani, wanaona kucheza Dhidi ya Brazil Itakuwa ni maandalizi tosha Kuelekea kulitetea taji lao, kwani wao ndio Mabingwa Watetezi.
.
– Mara ya Mwisho kukutana Kwa Nchi hizo Mbili Brazil walishinda 4-1, huku nahodha wao Neymar akiingia nyavuni Mara Mbili.
.
– Mechi hii Itakuwa ni kipimo kingine Kwa kocha wa Cameroon, Clarence Seedorf, ambaye kapewa kibarua hicho mwezi Agosti ambapo kaiongoza nchi hiyo katika mechi za sare dhidi ya Comoros na Malawi pia na mechi ya ushindi 1-0 Dhidi ya Malawi.
.
– Kwa kocha wa wa Brazil, Tite hii Itakuwa ni mechi yake ya kwanza akiwa Kama kocha mkuu kukutana Dhidi ya timu ya Taifa kutoka Bara la Afrika