Matatizo ya Madrid – Nini Shida? Perez? Kocha au wachezaji?
:
:
Real Madrid wamekuwa na mwanzo mbovu wa ligi kuliko wakati wowote kwenye historia yao, baada ya mechi 9, wana pointi 14, ushindi 4, sare 2, wamefungwa 3. Katika mechi 5 zilizopita wana goli 1 tu. Nini shida?
:
Yawezekana matatizo ya sasa kimatokeo si kitu kipya kwani hata msimu uliopita muda kama huu waliangusha pointi za kutosha njiani kwenye michezo dhidi ya Levante, Valencia na Rea Betis.
.
Lakini kipindi hicho bado Madrid ilikuwa na Zidane, mtu ambaye uwepo wake ulisaidia sana kuficha mapungufu ambayo Madrid walikuwa nayo muda mrefu .
Zidane kwa nyakati tofauti amewahi kushika nafasi zote zinazohusiana moja kwa moja na soka kwenye Real Madrid, kuanzia mchezaji mkubwa enzi zake, kocha wa timu za vijana, mkurugenzi wa ufundi na mtaalamu wa usajili, kocha msaidizi kwenye kikosi cha kwanza na kocha mkuu hapo baadae.
:
Kama mtaalamu wa usajili na mkurugenzi wa ufundi ni Zidane aliyecheza sehemu muhimu ya usajili wa watu kama Varane ambaye isingekua mfaransa huyu mwenye upara Varane alikua anaelekea OT, ni Zizzou ambaye alimshawishi Perez kukiukwa matakwa yake na kumsajili Isco toka Malaga huku Perez akimuona si galactico.
.
Akiwa kocha Zizzou hakutegemea sana mbinu bora na mifumo sahihi, aliamini kuwa ana wachezaji sahihi ambao uwezo waliokuwa nao ungetosha kushinda mechi yoyote.
Wakati Zizzou anaondoka sababu iliyotajwa ni kutokukubaliana na Perez juu ya mwelekeo wa timu kwenye upande wa usajili, Zidane aliona kuwa Madrid ina tatizo la wachezaji kubweteka na kunyanyua ari yao kwa mechi au michuano mikubwa na kudharau michezo midogo hasa kwenye ligi .
Leo hii Julen Lopetegui anaangushiwa jumba bovu katika mazingira ambayo wala hastahili lawama zozote.
.
Kuondoka kwa Zidane kulipaswa kuwakumbusha viongozi wa Real kuwa kiungo muhimu kwenye usajili. Walipaswa kuajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye angekua na jukumu la kuandaa mkakati wa muda mrefu.
:
Perez alidharau mchango wa CR7 aliyekuwa akifunga angalau magoli 50 kila msimu – akaacha kusajili mbadala.
.
Swali gumu kujibika ni hili, Je wakimfukuza kocha Julen Lopetegui hali itabadilika?
:
El Clasico live on @azamtvtz J’pili saa 12:15 jion