LiverPool Kuendelea kumkosa NABY KEITA

– Kiungo wa Kimataifa wa Guinea, Naby Keita ataendelea kukosekana katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya Liverpool baada ya kutopona majeraha yake aliyopata akiwa na timu yake ya Taifa.
.
– Kocha mkuu wa Majogoo hao, Jurgen Klopp Amethibitisha hii leo kuwa kiungo huyo atakuwa Nje wakati jeshi lake litakaposhuka Dimbani kukipiga Dhidi ya Cardiff City Wikendi hii Katika mechi ya Premier League..
.
– Pia Klopp Amesema wazi wataendelea kumkosa nahodha wao Jordan Henderson.
.
“[Keita na Henderson] wote hawatocheza kesho, lakini wapo katika hali nzuri ya kupona, lakini hawapo tayari kwa kesho” Klopp amethibitisha kwenye pre-match conference.