Yanga Sc: kumsajili beki wa kimataifa wa RWANDA

Imeripotiwa kuwa klabu ya Yanga ipo kwenye mazungumzo na meneja wa beki wa kimataifa wa Rwanda Abdul Rwatubyaye anayecheza klabu ya Rayon Sports ya Rwanda ili kumsajili kipindi cha usajili wa dirisha dogo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kuwa kamati ya Usajili ya klabu hiyo inataka kumuongeza beki huyo mwenye miaka 22 ili kuongeza nguvu kwenye eneo hilo.
Mpaka sasa beki huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Rayon Sports