Achana na burudani inayotolewa na kiungo fundi Cletus Chotta Chama ‘Triple C’, mwamba wa Lusaka katika kikosi cha Simba, beki Shomari Kapombe ndiye kinara wa ‘upishi’ wa mabao ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Kapombe beki mwenye uwezo wa kupanda na kushuka kwa kasi, ametengeneza mabao matano yaliyofungwa na Simba msimu huu.
Amekuwa katika kiwango bora na hakika anastahili pongezi za kipekee.
Afisa wa Habari wa Simba Haji Manara amesifu kiwango kinachoonyeshwa na beki huyo aliyerejea Simba msimu uliopita akitoka Azam Fc.
“Cloutus Chama kiuhalisia anacheza mpira wa kwenye play station,jamaa anajua hadi anakera! Wakati tunamsajili nilivyotamba sikueleweka,now tunaelewana”, ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram
“Na hivi kweli Kapombe anacheza ligi ya Bongo bado? Anaassist kuliko mabeki wengi wanaopuyanga kwenye Premier!
Simba na Barcelona ndio vitu vinavyoburudisha zaidi Duniani kando ya Pesa!”