Mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh amesema kiungo Ibrahim Ajib huenda akarejea kikosini kwenye mchezo wa Jumapili ijayo dhidi ya Ndanda Fc.
Ajib sambamba na Papi Tshishimbi wamekosa michezo miwili iliyopita dhidi ya KMC na Lipuli kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali.
Wakati Ajib akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, Tshishimbi alikuwa na matatizo ya goti.
Wawili hao walishindwa kutumika kwenye mchezo wa jana licha ya ripoti ya daktari kubainisha utimamu wa afya zao.
Yanga imefanikiwa kushinda michezo yote miwili waliyokosa viungo hao mahiri hivyo kudhihirisha kuwa timu hiyo haitegemei mchezaji mmoja tofauti na inavyodhaniwa na mashabiki wa timu pinzani