Full Time : Yanga 1-0 African Lyon

Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa kirafiki uliopigwa dimba la Uhuru leo Jumapili.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Pius Buswita kwenye dakika 43 kwa bao maridadi kabisa akiuvusha mpira juu ya mlinda lango aliyekuwa ametoka.

Kwenye mchezo wa leo Yanga iliwapa nafasi wachezaji wake ambao mara kwa mara wamekuwa hawapangwi kwenye kikosi cha kwanza.

Baada ya mchezo huo Yanga itashuka tena dimba la Uhuru Jumatano kuikabili Reha FC kabla ya kusafiri mkoani Lindi kucheza na Namungo Fc.

Michezo yote ni kwa ajili ya kukiandaa kikosi cha Yanga kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc utakaopigwa mkoani Shinyanga Novemba 22, 2018

Leave a comment