EPL: Manchester City vs Man United
.
:
Manchester City wanategemea kumrudisha Kun Aguero kikosini baada ya kumpa mapumziko katika mchezo wa UCL vs Shakhtar Donetsk.
Kevin de Bruyne, Eliaquim Mangala na Claudio Bravo wataendelea kuwa nje ya kikosi kutokana na majeruhi. :
Manchester United wataamua kumpa nafasi Lukaku kutokana na ushauri wa daktari kama atakuwa na utimamu wa kiafya.
:
United pia wana wasiwasi mkubwa juu ya utimamu aa kiafya wa Paul Pogba, ambaye hakufanya mazoezi Ijumaa na hata jana hakuonekana kambini katika hotel ya Lowry..
:
Diogo Dalot bado ataendelea kuwa nje – wakati nahodha Tony Valencia amepona na fiti kucheza, jumatano alisafiri na timu kwenda Italy.
:
:
Takwimu:
:
•Tangu walipopoteza Derby iliyopita mnamo April 2018, City wameshinda pointi 25 katika pointi 27 walizokuwa wakishindania kwenye uwanja wa Etihad, wamefunga magoli 32 na kuruhusu magoli manne tu.
:
•Manchester United hawajafungwa katika uwanja wa Etihad katika mechi 3 zilizopita, wameshinda 2 na kutoa sare 1.
:
•Endapo leo Manchester United watashinda – wataweka historia ya kushinda mechi mbili mfululizo katika uwanja aa Etihad kwa mara ya pili. :
•City wameshinda mechi mbili tu dhidi ya Manchester United katika mechi 8 zilizopita za mashindano yote, wamefungwa 4 na sare 2.
:
•Pep Guardiola hajawahi kupoteza mechi mbili mfululizo za ligi zilizochezwa uwanja wa nyumbani dhidi ya timu moja. Je Mourinho ataichafua rekodi hiyo leo usiku saa 1:30. Only on @dstvtanzania