Mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk na nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Mbwana Ally Samatta jana amecheza mchezo wake wa 100 katika ligi kuu nchini Ubelgiji, huku timu hiyo ikiendeleza rekodi ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Royal Excel Mouscron.
Samatta ambaye alianza katika kikosi cha jana, alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo licha ya kutofunga bao lolote.
Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza ligi ya Ubelgiji ikifikisha pointi 35 baada ya kutoka sare mechi tano kati ya mechi 15 ilizocheza, nyingine zote 10 ikishinda. Ambapo sasa inafuatiwa na Club Brugge yenye pointi 31 katika mechi 15 pia na sawa na Antwerp.