SAMIR NASRI IS BACK

SAMIR NASRI IS BACK
:
:
Unakumbuka Samir Nasri lakini? Nauliza mnamkumbuka vizuri? Kule Ufaransa anakumbukwa sana na kashfa yake ya kugoma kumpisha siti Thierry Henry kwenye basi la timu ya taifa. Inasemekana Henry alikuwa na siti yake maalum lakini Nasri alikaidi utaratibu huo kiasi cha kuitwa mtukutu ndani ya timu ya taifa.
:
Sasa anarudi tena EPL. Awamu hii anaeleka West Ham sasa. Taarifa zinasema anakamilisha vipimo vya afya.

Ni baada ya safari ndefu ya maisha ya kusuasua ya kisoka tokea alipoanza kutemwa timu ya taifa na Bwana Didier Deschamps. :
:
Amekumbwa na dhoruba nyingi ingiwemo adhabu ya kufungiwa miezi 18 ya kutokujihusisha na soka baada ya kusadikika kutumia madawa ya kusisimua misuli. :
:

Kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada ya kuvunja mkataba wa klabu kutoka Uturuki ya Antalyaspor.

Nasri mwenye miaka 31 anatarajia kupokea kiasi ya £80,000.

Hebu fikiria hii West Ham 🇨🇱 Manuel Pellegrini kocha
🇦🇷 Pablo Zabaleta
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Andy Carroll
🇲🇽 Javier Hernandez
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Jack Wilshere
🇫🇷 Samir Nasri

Leave a comment