BREAKING: Fulham Yamtimua kocha Mkuu wa klabu Hiyo

#BREAKING:..
– Klabu ya Fulham ya England imethibitisha kumtimua kazi ya ukocha mkuu wa Klabu yao kocha Slaviša Jokanović kufuatia muenendo mbovu wa Matokeo ya Ushindi Katika Klabu yao.
.
– Kocha Slaviša Jokanović ameiongoza Fulham kucheza mechi 12 za Ligi Kuu Uingereza, akipata Ushindi Mmoja tu, Sare Mbili na Kupokea vipigo Mara Tisa, pia wameruhusu kufungwa Magoli 31 Katika mechi zao zote 13 na kufunga mabao 11 tu.
.
– Mara Moja baada ya kutimua Kocha huyo, Mmiliki na Mwenyekiti wa Fulham Shahid Khan amemtangaza kocha, Claudio Ranieri kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo akichukua mikoba ya Slaviša Jokanović.
.
– Ranieri, ambaye aliiongoza Leicester City kutwaa taji la Premier League mwaka 2016, kapewa Mkataba wa Makubaliano ya Kuingoza Fulham Mpaka Mwisho wa Msimu huu.
.
– Ranieri Ana kazi nzito ya kuitoa Fulham mkiani mwa Msimamo wa Premier League wakiwa na pointi tano wakiwa Nafasi ya 20, mechi ijayo ya Fulham chini ya kocha mpya Itakuwa ni Katika Premier League Dhidi ya Southampton Siku ya November 24 Ndani ya Craven Cottage…

Credit @sokawaytz