AZAM YALAMBA MATAPISHI YAKE
Klabu ya Azam FC imeiandika barua ofisi ya Bodi ya Ligi ikiomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zichezwe katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Azam wametaja sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na uwanja wao (Azam Complex) kuwa mdogo kuingiza mashabiki na watazamaji.
Msimu uliopita 2017/18 zilichezwa mechi mbili (Azam vs Simba na Azam vs Yanga) kwenye uwanja wa Azam Complex, Azam wamekiri kulikuwepo changamoto kubwa iliyotokana na inada kubwa ya watazamaji na kupelekea wengine kukosa kuushuhudia mchezo huo jambo ambalo siyo zuri kwa maendeleo ya mpira wa miguu.
Barua hiyo imeandikwa November 15, 2018 na kusainiwa na Abdulkarim Amin ‘Popat’ Mtendaji Mkuu wa Azam FC.