Mlinzi wa kulia wa Simba na timu ya Taifa, Shomari Kapombe amepata majeraha nchini Afrika Kusini kwenye mazoezi ya Stars inayojiandaa kuikabili Lesotho keshokutwa.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba mapema leo imethibitisha kuhusu kuumia kwa Kapombe
“Mchezaji wetu Shomari Kapombe ameumia na hivyo hatacheza mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON 2019 kati ya Tanzania na Lesotho ambao utachezwa siku ya Jumapili 18/11/2018 nchini Lesotho,” imesema taarifa hiyo
Kuumia kwake ni pigo kwa Stars ambayo inasaka ushindi dhidi ya Lesotho katika mchezo wa raundi ya tano kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019