NIYONZIMA : Bado ana nafasi Simba Sc

Kiwango kilichoonyeshwa na kiungo Haruna Niyonzima jana kimedhihirisha mchezaji huyo bado ana sehemu yake kwenye kikosi cha Simba.

Niyonzima aliyecheza kwa dakika 83 mchezo wa kirafiki dhidi ya Nyasa Big Bulltes, alidhihirisha uwezo wake na kuwa miongoni mwa wachezaji walion’gara kwenye mchezo huo.

Mchezo huo uliopigwa dimba la Taifa ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana

Niyonzima amerejea katika kikosi cha Simba mwezi uliopita baada ya kutatua mgogoro baina yake na uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Tangu arajee kikosini bado hajaweza kumshawishi kocha Patrick Aussems kuweza kumtumia kwenye michezo ya ligi.

Lakini hali hiyo huenda ikabadilika kwenye michezo ijayo kutokana na juhudi kubwa anazoonyesha sasa.