Wakati Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Mnigeria Emmanuel Amunike, akisema haikuwa rahisi kuwafunga Cape Verde na kurejesha matumaini ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Cameroon mwakani, hesabu za Tanzania kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ziko mikononi mwetu.
Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde mwezi uliyopita, uliifanya Stars ifikishe alama tano na ushindi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Lesotho utaipeleka Stars Cameroon baada ya Uganda kuichapa Cape Verde bao 1-0 leo.
Uganda imefikisha alama 13 baada ya ushindi wa leo na kama Stars itashinda kesho itafikisha alama nane.
Alama hizo haziwezi kufikiwa na Cape Verde wala Lesotho hata zikishinda mchezo mmoja utakaokuwa umebaki.
Stars iliweka kambi nchini Afrika Kusini kwa takribani wiki nzima ikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili Novemba 18 huko Lesotho.
Tayari iko Lesotho ambapo leo jioni itajifua kwenye uwanja utakaopigwa mchezo huo kesho.
Amunike amesema wanakwenda Lesotho wakiwa na lengo moja tu la kuhakikisha wanaibuka na ushindi ambao utawahakikishia tiketi ya kufuzu AFCON 2019