MO: Aitakia kheri Taifa Stars

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘MO’ ameungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ili iweze kuibuka na ushindi huko Lesotho.

Ushindi utaiwezesha Stars kukata tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwakani mwezi wa sita nchini Cameroon.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, MO amesema anaamini ushindi utarudisha furaha ya Watanzania baada ya kukosa kushiriki fainali za AFCON kwa zaidi ya miaka 38.

“Nawatakiwa kila la kheri Taifa Stars katika mchezo wa leo dhidi ya Lesotho. Ushindi wa leo utarudisha furaha ya Watanzania ya kukosa kushiriki AFCON kwa miaka 38. Tunaamini mtafanya vizuri sababu nia tunayo na uwezo tunao. Mungu awe nanyi,” ameandika MO