Tanzani (U23) 3-1 Burundi (U23)

Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 23 imeshindwa kulinda ushindi wa mabao matatu baada ya kuondoshwa katika michuano ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 kwa vijana licha ya ushindi wa mabao 3-1.

Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 89 kabla Cedric Mavugo mdogo wa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Laudirt Mavugo kuifungia Burundi bao muhimu lililowapa tiketi ya kutinga raundi ya pili.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na Habibu Kiyombo (4′), Mbaraka Yusufu (43′) na Kihimbwa (70′)

Tanzania ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini ilishindwa kuzitumia vyema nafasi nyingi ilizotengeneza.