Mtibwa sugar 4-0 Dynamo

Mtibwa Sugar imeanza vyema michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) baada ya kuilaza Northern Dynamo kutoka Shelisheli kwa mabao 4-0.

Jaffar Kibaya amefunga mabao matatu ‘hat-trik’ kwenye mchezo huo huku bao la nne likifungwa na Riphat Msuya

Matokeo hayo yameiweka Mtibwa Sugar katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo wiki ijayo itasafiri kwenda Shelisheli kurudiana na timu hiyo.

Kesho Jumatano itakuwa zamu ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba ambao watashuka kwenye dimba la Taifa kuikabili Mbabane Swallows kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa(CAF CL), hatua ya awali

Mashabiki wa Simba na Watanzania wazalendo wanausubiri kwa hamu mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatahitajika zaidi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Uswatini wiki ijayo