
Mazembe imekuja nchini kwa kutumia ndege binafsi ambapo timu hiyo kabla ya kuja jijini Dar es salaam ilitua kwa muda mkoani Mbeya
Simba leo ilitarajiwa kucheza na JKT Tanzania mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Hata hivyo mchezo huo uliahirishwa baada ya mvua kubwa iliyonyesha mapema mkoani Morogoro kujaza maji kwenye uwanja wa Jamhuri
Simba sasa inaelekeza nguvu zake kuelekea mchezo dhidi ya TP Mazembe