
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Zahera amesema baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku mbili Mtwara, vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo wa leo
“Nafurahi tumefanya maandalizi mazuri. Wachezaji hawakupata matatizo tangu tulipowasili hapa Mtwara,” amesema
“Hali ya hewa ni joto sawa na Dar es salaam, hivyo haiwezi kuwa changamoto kwetu
“Juzi jioni tulifanya mazoezi ya kuondoa uchovu jana pia tulifanya mazoezi mepesi ya kunyoosha minofu. kikosi changu kipo sawa kuelekea mchezo wa leo”
Yanga inasaka ushindi muhimu leo ili iendelee kuchimbia kileleni mwa msimamo wa ligi