Simba inayo nafasi ya kufanya maajabu Congo

Katika michezo minne ya robo fainali ya ligi ya mabingwa iliyopigwa jana, ni Mamelodi Sundowns pekee iliyotumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Al Ahly

Horoya ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na Wydad Casablanca kama ilivyokuwa kwa Simba dhidi ya TP Mazembe

CS Constantine ilikubali kipigo cha mabao 3-2 nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi Esperance

Michezo ya marudiano inatarajiwa kupigwa wiki ijayo April 13

Wawakilishi wa Tanzania, Simba watasafiri Lubumbashi DR Congo kuikabili TP Mazembe itakayokuwa nyumbani

Kwenye mchezo huo wa marudiano Simba inahitaji matokeo ya aina mbili ili iweze kutinga nusu fainali

Ushindi au sare yoyote ya mabao itaihakikishia Simba kuingia nusu fainali

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanao uwezo wa kufuzu ugenini baada ya kufanya tathmini ya mchezo wa jana

Amesema watajipanga wakapambane ugenini kuhakikisha wanapata matokeo yanayoweza kuwapeleka hatua ya nusu fainali