Yanga yasogeza mbele Gala Dinner

Uongozi wa Yanga umeahirisha hafla ya chakula cha jioni (Gala Dinner) iliyokuwa limepangwa kufanyika Jumamosi ijayo, May 11 2019 ili kuwapa nafasi wadau wa klabu hiyo kushiriki katika mazishi ya Mwanachama wao marehemu Dk Reginald Mengi ambaye aliwahi kuifadhili Yanga miaka ya nyuma

Hafla hiyo sasa itafanyika May 18 Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

Mwili wa Dk Mengi unatarajiwa kuwasili Jumatatu ambapo utahifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele Jumamosi ya May 11, Machame mkoani Kilimanjaro