
Simba ina michezo mitatu mfululizo itakayopigwa uwanja wa Uhuru na kama watashinda yote, basi watatetea ubingwa kabla ya kuivaa Sevilla May 23 mchezo ambao unaweza kutumika kuwakabidhi taji
Baada ya mchezo dhidi ya Azam, mchezo unaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar kisha kumaliza na Ndanda Fc May 19
“Ushindi mchezo dhidi ya Azam ni muhimu. Matokeo hayo yatatuweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa,” amesema
“Azam ni timu nzuri, tuliwafunga kwenye mchezo wa kwanza. Tunahitaji kuwa katika kiwango bora ili tuwafunge tena”
Hata hivyo Aussems amesema Simba bado ina michezo mingi (sita) na lengo lao ni kushinda yote
“Mechi zote zilizobaki tunazichukulia kwa umuhimu uliosawa. Tunafahamu hazitakuwa nyepesi lakini tumedhamiria kutetea ubingwa hivyo tunahitaji matokeo a ushindi. Tutapambana kadiri ya uwezo wetu ili kufikia malengo”