Category: kimataifa
MATOKEO : Mechi za UEFA Leo USIKU
⚽ 06/03/2019 ⚽
🇪🇺 🏆 UEFA CL
⚽ PSG 1-3 Man Utd
⚽ FC Porto AS 3-1 Roma


MECHI ZINGINE
🇫🇷🏆 Coupe de France
⚽ Vitré 0-2 Nantes
🏆 Supercopa de Catalunya
⚽ Barca 0-1 Girona
Kikosi Cha Man U vs PSG
Kikosi cha vijana wa Ole Gunnar Solskjaer vs PSG
MBWANA SAMMATA : Azidi kukimbiza ULAYA
Mchezaji MBWANA SAMMATA Ameingia kwenye Top 5 ya waliofunga magoli mengi Kwenye Michuano Yote


Credit: #Sokaonline
Baada ya kutolewa Champions League, Real Madrid wamepata pigo jingine
Wakatia club ya Real Madrid pamoja na mashabiki wao wakiwa katika majonzi mazito kutokana na timu yao kuondolewa mapema katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 tofauti na ilivyozoeleka, kuna habari mbaya pia imeripotiwa leo kuhusiana na moja kati ya wachezaji wao ambaye wanamtegemea pia.

Club ya Real Madrid leo imepokea taarifa za kuthibitika kuwa itamkosa kwa miezi miwili Vinicius Jr, hiyo inatokana na staa huyo kupata majeraha wakati wa mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Ajax mchezo ambao umemalizika kwa Real Madrid kuvuliwa Ubingwa na kuaga rasmi michuano hiyo 4-1 (agg 5-3).

Jeraha alilolipata Vinicius Jr mwenye umri wa miaka 18 kitaalam linajulikana kwa jina la torn ligaments, kama utakuwa unakumbuka vizuri Vinicius Jr alijiunga na Real Madrid 2018 akitokea Flamengo lakini amepata jeraha kubwa litakalomuweka nje kwa kipindi cha miezi miwili
Full Time: Real Madrid 1-4 Ajax #UEFA
Full Time: Real Madrid 1- 4 Ajax #UEFA Champion League




Duuuh
PICHA: Neymar kwenye penzi jipya na staa wa Pop?

Msanii wa muziki wa Pop Anitta ameanza kuingia katika tuhuma za kudaiwa kutoka kimapenzi na mwanasoka wa Brazil ambaye pia ni mchezaji wa Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa Neymar, Anitta ameanza kuhusishwa kuwa katika mahusiano na Neymar baada ya ukaribu kuzidi.

Anitta na Neymar wameonekana wakiwa beneti katika jiji la Rio De Janeiro nchini Brazil, ukaribu ambao umeanza kuzua utata mitandaoni kuwa inawezekana wawili hao kuna kitu kinaendelea, Anitta ni moja kati ya wasanii wa Pop maarufu nchini Brazil na Amerika ya Kusini na amekuwa akifanya kazi zake kwa kutumia lugha ya kireno.

Neymar na Anitta wakiwa Rio De Janeiro katika tamasha la Sambadrone wameonekana wakikumbatiana na ku-kiss kitu ambacho kinaaminika kuwa kuna uwezekano wawili hao wakawa mapenzini, Neymar alithibitika kuachana na girlfriend wake ambaye ni muigizaji maarufu nchini Brazil Bruna Marquezine toka October 2018.
Jose Mourinho anatamani kurudi Chelsea sio Real Madrid

Baada ya kufukuzwa kazi na uongozi wa Man Unitedkwa kocha wa kireno Jose Mourinho, mashabiki wengi wa soka wanatamani kujua mreno huyo ana mpango wa kwenda timu gani kuifundisha tena licha ya kuhusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo club yake ya zamani ya Real Madrid.
Mourinho alipata nafasi ya kufanya mahojiano na beINSports na alipoulizwa kama ana mpango wa kurudi kufanya kazi katika club aliyowahi kufanya kazi awali alijibu kuwa ndio ni furaha na fahari kubwa kwake kurudi kama watakuwa wameona umuhimu wake na kumuhitaji kama ni Chelsea lakini kwa Real Madrid hapana.

“Kurudi timu ambayo nilikuwa awali sio tatizo kama wameniita tena kama naona ni wakati sahihi, kuna mfumo sahihi na malengo ya mbali hakuna shida kwa mimi kurudi katika club ambayo nimewahi kufanya kazi awali, nafikiri ni fahari kubwa wakati club uliyowahi kuifanyia kazi kukuita tena”>>> Jose Mourinho
“Lakini kwa sasa nina hamu ya kurudi Chelsea sio Real Madrid, hapana naipenda Hispania lakini sichagua timu kwa sababu ya nchi au hali ya hewa”>>> Jose Mourinho
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho amewahi kufanya kazi na vilabu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti ikiwemo Real Madrid na Chelsea, Chelsea amewahi kuifundisha katika vipindi viwili (2004-2007) na (2013-2015) wakati Real Madrid amewahi kuifundisha kwa miaka mitatu (2010-2013).
Full Time Dortmund 0-1 Tottenham #UEFA
Full Time
Dortmund 0-1 Tottenham
(Agg. 0-4)
#UCL
Real Madrid kavuliwa Ubingwa wa UEFA Champions League nyumbani kwake

Hatimae muda wa furaha umeisha ndani ya club ya Real Madrid ikiwa ni siku moja imepita toka kiungo wa timu hiyo Luka Modric kukiri kuwa timu yao haina mbadala wa Cristiano Ronaldo na wanamkumbuka sana, pia Real Madrid imempoteza kocha wao aliyewaweka katika rekodi ya kihistori na kuwapa Ubingwa wa UEFA Champions League mara tatu.

Real Madrid ikiwa inacheza msimu wake wa kwanza wa UEFA Champions League bila uwepo wa Cristiano Ronaldo wamejikuta wakitolewa katika michuano hiyo na kuvuliwa Ubingwa huo baada ya kutwaa mara tatu mfululizo, kufuatia kipigo cha magoli 4-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu, ushindi wa ugenini wa 2-1 waliowafunga Ajax wiki mbili zilizopita haujawa na msaada kwao.

Hivyo Real Madrid wamejikuta wanaondolewa katika michuano hiyo kwa ushindi wa Ajax wa jumla ya magoli 5-3, Real Madrid baada ya kutolewa leo katika hatua ya 16 bora ndio wanakuwa wametolewa kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo katika hatua ya mapema zaidi, kwani kwa miaka 9 toka (2010-2011) hawajawahi kutolewa hatua ya 16 bora au robo fainali.


Matokeo ya game za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa March 5 2019, Ajax na Tottenham zimefuzu robo fainali.









