HIMID MAO ACHEZA MECHI YOTE TIMU YAKE YACHAPWA 4-0 NA AL AHLY LIGI YA MISRI

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, Petrojet FC ikichapwa mabao 4-0 na Al Ahly katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Petrosport mjini Cairo.
Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Junior Ajayi dakika ya nane akimalizia pasi ya Nasser Maher, Marwan Mohsen dakika ya 31 akimalizia pasi ya Geraldo aliyefunga la tatu dakika ya 69 kwa pasi ya Ali Maaloul na Karim Nedved aliyefunga la tano dakika ya 75.
Nedved aliyefunga akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la pili la Al Ahly, Marwan Mohsen angeweza kufunga mabao zaidi kama angetumia vyema nafasi nyingine alizopata.
Kwa ushindi huo, Al Ahly inafikisha pointi 51 baada ya kucheza mechi 22, ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Zamalek inayoongoza kwa pointi zake 52 za mechi 21

MAN UNITED Yamfuatilia Kiungi Huyu

Klabu ya Manchester United ya Uingereza inamfuatilia kiungo wa kati wa Barcelona na timu ya Taifa Croatia Ivan Rakitic, 30 ifikapo mwishoni mwa msimu huu (Mail)Hata hivyo huenda wakamkosa kutokana na yeye kusema kamwe kwasasa hawezi kuondoka klabuni hapo bado anatamani kuendelea kukipiga kwenye miamba hiyo ya Hispania