Mkataba wa DDG unavyowaumiza kichwa United – Juventus huenda wakamsaini buree.
:
:
Jose Mourinho amesema hana uhakika juu ya golikipa wake David De Gea kusaini mkataba mpya, DDG mkataba wake na United unaishia mwishoni mwa msimu ujao na taarifa mpya zinadai Juventus ambao wana uzoefu na kusajili wachezaji ‘huru’ wameanza kuvizia saini ya De Gea
.
.
Golikipa huyo mwenye miaka 27 mkataba wake wa sasa unaishia mwishoni mwa msimu wa 2019/20, na sasa inaonekana wazi kwamba Juventus wapo tayari kumsubiri amalizane na United na kumsaini bure kama ilivyokuwa kwa Paul Pogba mwaka 2012
.
.
De Gea amekuwa akitegemewa kusaini mkataba mpya na United kwa muda mrefu sasa tangu Thibaut Courtois alipojiunga na Real Madrid wakati wa kiangazi, lakini mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na Mourinho leo amesema hana uhakika na kukamilika kwa dili jipya na United na taarifa mpya zinadai Juventus ambao wameshinda Serie A kwa miaka 7 mfululizo wapo katika nafasi nzuri ya kumshawishi DDG kuhamia Italia
.
.
Chanzo cha karibu na Manchester United kimesema: “De Gea amecheza dhidi ya waajiri wake wajao jumanne iliyopita. Endapo United hawatomuuza dirisha kubwa likifunguliwa, basi Juventus watasubiri mpaka mkataba wake umalizike.”
.
Inaelezwa DDG ambaye alishindwa kuhamia Madrid miaka 3 iliyopita kutokana fax machine ya Madrid kusumbua, ameshindwa kusaini mkataba mpya na United kwasababu anaona muelekeo wa klabu sio mzuri, umri wake unasogea na hakuna mafanikio ya maana aliyopata, hivyo sasa anaangalia machaguo tofauti kabla ya kuamua kukubali au kukataa kusaini mkataba mpya na United.
:
Juventus ambayo imetoka kumsaini Cristiano Ronaldo kwa dau la £99m wana utayari wa kuwalipa United ikiwa klabu hiyo itakubali kumuuza DDG, au watamsubiri mpaka mkataba wake umalizike na kumsaini bure ili aje kuziba pengo liloachwa wazi na Gigi Buffon aliyejiunga na PSG.
:
Katika miaka ya hivi karibuni, Juventus imefanikiwa kusajili bure wachezaji wakubwa ambao wameisadia kwa kiasi kikubwa kuirudisha katika listi ya vilabu bora duniani.
:
Wachezaji waliosajiliwa bure na Juventus
✅ 2009: Fabio Cannavaro
✅ 2011: Andrea Pirlo
✅ 2012: Paul Pogba
✅ 2013: Fernando Llorente
✅ 2014: Kingsley Coman
✅ 2015: Sami Khedira