SAMATTA AVUNJA REKODI GENK

SAMATTA KWENYE ORODHA YA WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE GENK

Katikati ya juma hili aliyekuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani na Nyota wakimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta [Samagoal, The Champion boy] pamoja na mchezaji bora wa Afrika Mohamed Sallah [Egyptian King] wamefanikiwa kufikisha mabao 50 ndani ya vilabu vyao.

Mabao mawili ya @samagoal77 dhidi ya golikipa wa zamani wa Liverpool aliyewahi pia kucheza na Mo Sallah Karius yalitimiza idadi ya mabao 50 kwa Samatta. Samatta sasa anaingia kwenye kumbukumbu za wachezaji waliowahi kufunga mabao 50 katika historia ya klabu hiyo.

@mosalah ameweka rekodi ya kufunga mabao 50 ndani ya mechi chache zaidi ikiwa ni mechi 65 tu. Mo Salah sasa anakuwa mfungaji bora ndani ya Liverpool kutoka Afrika na anakuwa mfungaji bora namba 20 katika historia ya wafungaji bora Liverpool.

Mbwana Samatta amebakiza mabao 9 kufikia rekodi ya mfungaji bora namba 5 wa muda wote wa Genk. Samatta anashika namba 6 akiwa na mabao 50 na ndiye mchezaji pekee kutoka Afrika mwenye mabao mengi ndani ya Genk.

Samatta anaifukuzia rekodi ya baba yake Divock Origi, Mzee Mike Origi ambaye anashikilia rekodi ya mchezaji pekee kutoka afrika mashariki mwenye mabao mengi ndani ya ligi kuu Ubelgiji [33]. Samatta kufikia sasa ana mabao 24 tu ndani ya Ubelgiji.
Ikumbukwe pia Origi aliwahi kucheza Genk mwaka 1998 na alifunga mabao 20 katika michezo 80.

Kufikia hivi sasa Samatta msimu huu ndani ya ligi kuu amehusika katika magoli 11 michezo 8 [Magoli 9 na asisst 2]

Samatta msimu huu amehusika magoli 18 kwenye michezo 18. [Magoli 16 na assists 2]
. .
Kwa Ujumla Mpaka sasa Samatta amehusika mabao 63 katika michezo 130, [Mabao 50 na Asissts 13].
.
. πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ