Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa bodi ya Simba Hussein Kitta amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa, jambo la kwanza itakuwa ni kuwaelewesha wanachama juu ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.
:
KWA NINI AMECHUKUA FOMU KUGOMBEA?
Wakati umefika kwa sababu nimekuwa nikifatilia masuala ya mpira kwa siku nyingi, nimekuwa kiongozi kwenye makundi madogomadoo kama tawi la Simba Makini, baada ya haya mabadiliko ya mfumo nimeona unaendana na fikra za Simba Makini nimeona naweza ku-fit kwenye mfumo wa sasa.
:
ATAIFANYIA NINI SIMBA?
Mambo ya kufanya ni mengi, pamoja na kutoa mchango wangu katika masuala ya mpira yapo zaidi ya mpira ambayo mimi nina uwezo nayo kwa sababu ya taaluma yangu. Kitaaluma mimi ni mwanasheria ni mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam.
:
Kazi ya kwanza kabisa ni kuelewesha wanasimba juu ya huu mfumo mpya kwa sababu ukimsimamisha mtu barabarani ukamuuliza kuhusu huu mfumo atashindwa kukujibu kwa hiyo natakiwa kuhakikisha watu wanaelewa ili yanayokwenda kufanyika waelewe yanafanyika kwa sababu ya mfumo mpya.
:
Kule kwenye bodi ndio ambapo mikakati mikubwa inapangwa sehemu ambayo mwelekeo wa klabu na shughuli zake unatengenezwa kwa hiyo nakusudia nitakapokuwa pale kupitia uzoefu wangu katika masuala ya mpira na taaluma yangu nitavichanganya pamoja ili vitusaidie kuijenga Simba imara.
:
Anakuja mwekezaji Mohammed Dewji anaweka bilioni 20, ile bodi itakuwa na watu mchanganyiko watu kutoka upande wa klabu na wengine kutoka upande wa mwekezaji. Sitegemei mtu aweke bilioni 20 halafu alete watu dhaifu kwenye bodi kwa hiyo ninaamini nina uwezo wa kuwawakilisha wanachama wa Simba kwenye bodi katika kusimamia maslahi yao kwa hoja ambazo naweza kuzisimamia.
:
SERA ANAYOINGIA NAYO
Naingia na sera ya kufanya kazi pamoja na wenzangu wa bodi kwa maslahi ya wanachama ambao wamenichagua.
:
Simba sasa hivi inakuwa kampuni (Simba Sports Club LTD) kampuni huwa zinakuwa na malengo ambayo tayari yameandikwa kwenhe document ya kuanzisha kampuni, kwa hiyo nitahakikisha nayasimamia malengo yote lakini pia kuna wanachama ambao wamenituma na Simba ina historia yake ambayo hiki chombo kimpya kinachokuja kitahakikisha pamoja na mabadiliko, haipotezi kule ilikotoka.