YANGA: Yatoa tamko kuhusu BANKA

Baada ya TFF kubainisha kuwa kiungo Mohammed Issa Banka amefungiwa miezi 14 baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua mwili (bangi), uongozi wa Yanga unasubiri barua rasmi kutoka TFF ili uweze kutoa tamko.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema baada ya kutolewa kwa taarisa hiyo leo, wanasubiri barua rasmi kutoka TFF ili waweze kutoa tamko la timu.

“Taarifa imetoka leo, hivyo tunasubiri barua rasmi kutoka TFF ili tuzungumze”

“Hata hivyo, hatuwezi kusema kama Banka ameonewa au la kutokana na mazingira ya kesi hiyo. Kwani ushahidi ukiwemo vipimo vilichukuliwa pamoja utetezi wa mchezaji mwenyewe ambaye amekiri kosa”

Banka ametua Yanga akitokea Mtibwa Sugar hata hivyo hakuwahi kujiunga na timu hiyo.

Adhabu yake imeanza Disemba 2017 na itamalizika Februari 02, 2019.

Wakati anajiunga Yanga alisaini mkataba wa miaka mitatu. Anaweza kuanza kutumikia Yanga baada ya miezi minne.

Hata hivyo anaweza akaruhusiwa kuanza kujifua na Yanga kuanzia mwezi Disemba