YANGA: Kusajili Jembe Hili

Yanga imekuwa kwenye mazungumzo na beki kisiki wa Rayon Sports, ambaye ni nahodha wa timu hiyo, Abdul Rwatubyaye

Wakala wa mchezaji huyo alikiri kuwa na mazungumzo na uongozi wa Yanga lakini pia akisema klabu ya Simba nayo imeulizia upatikanaji wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23

Kulingana na taarifa zinazoripotiwa na vyombo vya habari nchini Rwanda, Rayon Sport iko tayari kumuachia Abdul kwa kitita cha Mil 80

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amekuwa kwenye mazungumzo na wakala wa mchezaji huku ikielezwa tayari pande zote zimefikia makubaliano juu ya usajili wa beki huyo.

Inaelezwa uko uwezekano mkubwa kwa beki huyo kutua Yanga mapema tu dirisha la usajili litakapofunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo

Yanga pia imemalizana na mshambuliaji wake wa zamani Obrey Chirwa ambaye awali aliwekewa ngumu na kocha wa timu hiyo Miwnyi Zahera