DANGOTE AWATOLEA TENA UVIVU ARSENAL.
Tokea mwaka 2015 ilisemekana kuwa Bilionea Aliko Dangote ana ndoto za kuimiliki Arsenal. Yeye anasema ni mshabiki damu damu wa Arsenal na mara kadhaa alikuwa akimkosoa sana meneja wa zamani wa Arsenal Bw Arsene Wenger:
:
Bilionea huyo ameeleza hisia zake kuwa bado ndoto zake za kuinunua Arsenal zipo pale pale. Ingawa amesisitiza kuwa ndoto zake hizi zinaelekea ukingoni. Hata hivyo amesema kuwa kama Arsenal wanaringia ofa yake basi atanunua klabu nyingine:
:
“Naipenda sana Arsenal. Kama hawapo tayari kuiuza basi nitanunua klabu nyingine” :
:
“Mwaka jana nilitangaza wazi kuwa baada ya kukamilika kiwanda changu cha mafuta, mapato yataongezeka mpaka kufikia dola Bilioni 22 hivyo haitaniathiri kiuchumi” :
:
Dangote mwezi agosti mwaka huu alitajwa na na jarida la Forbes kuwa ana utajiri wa Paundi bilion 11.