Stars Yazidi Kujifua AFRIKA KUSINI

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo Jumatano imefanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Celtic Bloemfontein nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu Fainali za AFCON dhidi ya Lesotho utakaofanyika Maseru Novemba 18,2018.

Kikosi cha Stars kimetua jana nchini Afrika Kusini kuweka kambi hiyo maalum ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Stars inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L ikiwa imejikusanyia alama tano baada ya kushuka dimbani mara nne.

Uganda inayoongoza kundi L, iko katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu ikiwa na alama 10 wakati Cape Verde iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne.

Lesotho inashika mkia katika msimamo wa kundi L ikiwa na alama mbili.

Tanzania, Lesotho na Cape Verde zinawania nafasi ya pili.

Kama Stars itapata ushindi dhidi ya Lesotho halafu Cape Verde ikafungwa na Uganda basi Stars itafuzu sambamba na Uganda.

Leave a comment