TFF yawatahadharisha Wanaopanga kuvuruga mchakato wa UCHAGUZI Yanga

Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TFF Malangwe Ally Mchungahela amesema wanazo taarifa kuwa kuna wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga kwa kushirikiana na baadhi ya Wanachama wamepanga kuitisha Mkutano kesho Jumapili kutangaza kumtambua Yusufu Manji kuwa Mwenyekiti halali wa Yanga na kupinga uchaguzi wa kujaza nafasi yake.

TFF imewatahadharisha wote wanaopanga ajenda hiyo na kusisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi kwa nafasi zote zilizotangazwa utaendelea kama ulivyopangwa.

Mchungahela amesema wote wanatakaoshiriki katika ajenda hiyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na TFF bila ya kujali nafasi zao

Aidha, kutokana na kuchelewa kwa zoezi la utolewaji wa fomu, zoezi hilo sasa litafikia tamati Jumatano Novemba 14 baada ya TFF kuongeza siku moja

Leave a comment