Mshambuliaji wa Fc Barcelona na raia wa Ufaransa Ousmane Dembele ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka kunako klabu hiyo ifikapo mwezi January kwenda Arsenal ambayo imehitaji nia ya kumsajili (Daily Mail). .
.
Dembele hajawa na wakati mzuri tangu alipojiunga Barcelona akitokea Borussia Dortmund kutokana na kushindwa kuendeleza kasi yake aliyoanza nayo akiwa BundesLiga. .
.
Katika hatua nyingine, endapo Dembele ataondoka Barcelona huenda Barcelona wakaanza mchakato mapema wa kumrudisha mchezaji wake wa zamani Neymar ili kuchukua nafasi ya Dembele kama baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania vinavyoripoti.
#sokaUpdates